29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

‘CHF iliyoboreshwa kutoa huduma za uhakika’

TIGANYA VINCENT – RS TABORA

SERIKALI mkoani Tabora imewahakikishia wakazi wake kuwa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF) utatoa huduma ya uhakika ambayo itapendwa na kila mwanachama wa mfuko huo.

Mbali ya kutolewa huduma ya uhakika, pia CHF iliyoboreshwa  itahudumia idadi kubwa zaidi ya wanafamilia inayofikia watu sita ambao kila mmoja atakuwa na kitambulisho chake.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora,  Msalika Makungu baada ya kupokea vifaa vya uandikishaji wanachama wa CHF iliyoboreshwa kwa ajili ya huduma hiyo itakayoanza kutolewa Januari 12,  mwakani .

Aliwataka wananchi kujiunga kwa wingi kwa vile watapata manufaa makubwa wao na wategemezi wao katika kupata huduma bora ya afya.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Tausi Yunge, alisema uhakika wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma katika mkoa wa Tabora ni mzuri kwa vile sasa umefikia asilimia 92.

Alisema watakaojiunga na CHF iliyoboreshwa hawatakuwa na tatizo la dawa na kwamba zile ambazo zitakosekana utaratibu unawekwa ili zipatikane.

Naye Mratibu wa CHF iliyoboreshwa Mkoa wa Tabora, Baraka Makona, alisema uzinduzi rasmi wa mfuko huo utafanyika Januari 12 mwakani na siku moja baadae wanachama watakaokuwa wamejiunga wataanza kupata huduma.

Kiongozi wa Asasi ya Tuimarishe Afya, HPSS, Ally Kebwe, alisema CHF iliyoboreshwa itakuwa na idadi kubwa ya madawa kwa vlle huduma zaidi zitakuwa zikitolewa tofauti na zamani.

HPSS ndio iliyotoa vifaa vya uandikishaji Mkoa waTabora na kutoa mafunzo kwa waandikishaji wapatao 873.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles