25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Chenge aagiza serikali kutoa taarifa kupotea kwa Mdude, Masauni asema polisi wameanza uchunguzi

Arodia Peter, Dodoma

Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, ameitaka Serikali kufuatilia na kutoa taarifa za kutekwa kwa kijana na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagawa ambaye anadaiwa kutekwa.

Mdude anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana kwenye ofisi yake Mbozi, mkoani Songwe juzi, Mei 4 wakiwa na silaha za moto.

Chenge ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Mei 6, wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyetoa hoja ya kuahirisha Bunge kwa kutumia kanuni ya 64 kuhusu kujadili jambo la dharura.

Katika hoja yake, Msigwa alisema hivi karibuni kumekuwapo na matukio ya watu kutekwa, kupotea na hata kuuawa, huku akitolea mfano madai ya kutekwa kwa kada wa chama hicho, Mdude.

Akitoa maelezo ya hoja hiyo, Chenge ameitaka Serikali kutolea ufafanuzi jambo hilo.

“Ni kweli suala lolote linalohusu uhai wa binadamu, itakuwa vizuri Serikali itoe maelezo ili wananchi wajue hali ilivyo,” amesema Chenge.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusufu Masauni amesema Jeshi la Polisi limeanza kufanyia uchunguzi tangu jana, Mei 5, na wameongeza nguvu kutoka makao makuu ya jeshi hilo.

Aidha Masauni ameomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kuhusu utata wa tukio hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles