24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema waenda kujichimbia Mwanza

DSC008091Na Mwandishi Wetu, Dar

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kuanza vikao vyake vya ngazi ya juu mkoani Mwanza  kesho.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa chama hicho jana, Tumaini Makene ilisema kuanzia kesho wajumbe wa sekretarieti watawasili kwa ajili ya maandalizi ya vikao vinavyofuata.

“Kuanzia Machi 9, mwaka huu kutakuwa na kikao cha sekretarieti ya chama ambacho kitakuwa chini ya uenyekiti wa Kaimu Katibu Mkuu, Salum Mwalim,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema Machi 10 na 11, kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu kikifuatiwa na kikao cha Baraza Kuu la chama.

Baada ya kikao hicho, Machi 13 kutakuwa na Kamati Kuu na baadae mkutano wa hadhara. Siku inayofuata kutafanyika kikao cha sekretarieti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles