28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘Cannavaro’: Ushindi umetupa raha ya ubingwa

Nadir Haroub ‘CannavaroNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

NAHODHA wa timu ya soka ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema ushindi wa mabao 2-0 waliopata juzi dhidi ya Mbeya City umedhihirisha rasmi kuwa wao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wa juzi uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya, ‘Cannavaro’ aliwaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Jumamosi kushangilia ubingwa.

Jumamosi mabingwa hao wanatarajia kucheza mechi nyingine ya ligi dhidi ya Ndanda FC itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam badala ya Nangwanda Sijaona, Mtwara baada ya Yanga kuomba mabadiliko yafanyike ili waweze kukabidhiwa kombe.

Hata hivyo, ‘Cannavaro’ alisifia kiwango kilichoonyeshwa na Mbeya City katika mchezo wa juzi akidai kuwa kama wachezaji wataendelea kujituma kwa msimu ujao timu hiyo itaweza kushika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

“Licha ya kuwafunga na kuibuka na ushindi ugenini, wapinzani wetu wamecheza kwa kiwango cha juu ambacho kama watakiendeleza kwa msimu ujao timu yao itafanya vizuri na kushika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi,” alisema.

Yanga walitangazwa kuwa mabingwa msimu huu Jumapili iliyopita baada ya mahasimu wao Simba kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles