26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Michezo ya jadi wakabidhi rasimu BMT

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limepokea mapendekezo ya jina na rasimu ya kwanza ya katiba ya chombo kimoja kutoka katika Kamati Kuu iliyoagizwa kuunda na kusimamia michezo ya jadi nchini.

Mwenyekiti wa kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe kumi, Mohamed Kazingumbe, alikabidhi rasimu hiyo jijini Dar es Salaam jana kwa Ofisa Maendeleo ya Michezo wa baraza hilo, Milinde Mahona.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mahona alisema BMT ilitoa agizo katika kikao cha baraza kilichofanyika Aprili 22 mwaka huu likitaka Chama cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) na Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania (Shimbata) kukamilisha rasimu ili kurahisisha kazi ya kuunda chombo kimoja kitakachosimamia michezo ya jadi nchini.

“Katika kikao kilichopita Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohamedi Kiganya, aliagiza taasisi hizi mbili zivunjwe ili kiundwe chombo kimoja cha kusimamia michezo ya jadi na ambapo kila mchezo utajitegemea na kuwajibika kwa chombo kimoja,” alisema Milinde.

Naye Mohamed Kazingumbe alisema kamati hiyo pia imependekeza jina la umoja huo kuwa ni Shirikisho la Michezo ya Jadi Tanzania, (Shimijata) na kudai kuwa kamati hiyo ilihakikisha kuwa haikosei kwa kuwashirikisha na wadau wengine wakiwemo wanasheria.

Aidha, BMT imeiagiza Kamati Kuu kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu katiba zote za kusimamia michezo ya jadi nchini zinakuwa na chombo kimoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles