27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Wambura apitishwa kugombea FAM

wamburaNA SHOMARI BINDA, MUSOMA

KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM), imempitisha Michael Wambura kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho na kuondoa jina la mpinzani wake, Valence Mayenga ambaye anadaiwa kutokidhi vigezo.

Akizungumza jana mjini hapa kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi huo, mwenyekiti wa kamati, Ostack Mligo, alisema wagombea 16 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali walifanyiwa usaili ambapo baadhi waliondolewa.

Alisema wagombea wawili kati ya 16 waliowania nafasi mbalimbali waliondolewa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo lakini wanaruhusiwa kukata rufaa katika vyombo vya juu vinavyosimamia soka.

Mligo alisema kwenye nafasi ya mwenyekiti  Wambura alipitishwa lakini Mayenga aliondolewa kwa kukosa kigezo namba tano ambacho anatakiwa kuwa na uzoefu wa kuongoza klabu ya ligi za juu au chama cha soka kwa kipindi cha miaka mitano.

Aliyepitishwa kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti ni Magati Zambeli baada ya mpinzani wake Barnaba Makaranga kuondolewa kwa madai kuwa majina yake kwenye cheti cha kuzaliwa na elimu yalikuwa tofauti.

Waliopita kwenye nafasi ya katibu ni Silas Mziba, Revocatus Kuboja na Benard Sipila na hakuna mgombea aliyejitokeza kuwania nafasi ya katibu msaidizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles