27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mashabiki wampa Mahrez uchezaji bora

LONDON, ENGLAND

NYOTA wa klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez, ametwaa tuzo ya uchezaji bora wa mwaka baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa klabu hiyo.

Mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa kwa kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini England, hivyo mashabiki wa klabu hiyo wamemchagua mchezaji huyo juzi katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa King Power.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Algeria, amewashukuru mashabiki wake kwa kuutambua mchango wake ndani ya klabu hiyo na amewaahidi makubwa msimu ujao.

“Najisikia kuwa na furaha kubwa kupigiwa kura na mashabiki wangu, siku zote mashabiki wana nafasi kubwa katika klabu kupata ushindi, napenda kutumia nafasi hii kuwaahidi kwamba nitaendelea kujituma msimu ujao kwa ajili ya kuipa mataji mengine msimu ujao,” alisema Mahrez.

Wakati huo huo mashabiki hao walimpa tuzo ya bao bora mshambuliaji wao, Jamie Vardy, alilofunga katika mchezo dhidi ya Liverpool, pia waliipa tuzo timu yao kwa kiwango bora walichokionesha kwenye mchezo wao dhidi ya Manchester City ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Etihad, Leicester ilishinda mabao 3-1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles