22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

‘Bwawa la Nyerere lafikia ujazo wa lita bilioni 6 za maji’-Makamba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali imesema inaridhishwa na kasi ya Ujazaji maji Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power unaondelea.

Hayo yameelezwa leo Aprili 25, 2023 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba ambapo amesema kuwa kwa sasa ujazo wa maji umefika lita bilioni Sita huku kukiwa kumebaki mita 13 tu, kufikia kiwango cha Maji yatakayoweza kuzungusha mitambo ya kufua umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa kiwango hiko ni kizuri na kimezidi matarajio yaliyokuwepo awali wakati wa uzinduzi wa ujazaji maji uliofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kusema:

“Maendeleo mazuri ingawa kazi bado ipo. Kwa mujibu wa takwimu, wiki mbili zilizopita kiwango maji yameingia mengi kuliko yaliyoleta mafuriko 2019/2020. Hii maana yake neema iliyopo kwa sasa zile athari za mafuriko hazipo tena. Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko. Kwa sasa tuko asimilia 86 wakati Mhe. Rais Samia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37,” amesema Makamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles