22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Waislam Iramba wampongeza Dk. Mwigulu

Na Seif Takaza, Singida

WAISLAAM wilayani Iramba Mkoa wa Singida wamemshukuru Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Dk. Mwigulu Nchemba kwa sadaka yake kwa kuwafuturisha Waislaam katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Shukurani hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa BAKWATA Wilaya ya Iramba Sheikh Ali Katembo katika Baraza la IED FITRI liliofanyika juzi kikata katika Kitongoji Mgunga Kijiji cha Masagi Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui.

Sheikh Katembo ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Mtoa amesema Waislaam wilayani Iramba wamefarijika sana kwa kupata msaada wa tende na kwa ajili ya futari na mchele  hivyo Waislaam wanakuombea dua kwa cheo ulicho nacho uendelee kuwatumikia wananchi  wa Tanzania  .

“Kwa heshimana kwa uwezo wake Allah napenda nichukue fursa hii kukushukuru na kukupongeza kwa futari katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa niaba ya Waislaam wa Wilaya ya Iramba tunakuombea dua Mungu akubariki uwe na Siha njema halikadhalika tunamuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa hili kuwa na amani na utulivu,” alisema Sheikh Katemmbo.

Sheikh Katembo alisema kuwa anaiomba Serikali kuwachukulia vijana wanaokweda nje ya maadili kwa kupiga vita ushoga na usagaji pamoja na ndoa ya jinsia moja.

“Ni vitendo vya aibu vinavyofanywa na vijana wa sasa kila mmoja wetu aweze kukemea vitendo hivyo ambavyo  viko kinyume na vitabu vya Mwenyeezi Mungu na kinyume na maadili na tamaduni zza  makabila yetu,” alisisitiza Sheikh Katembo.

Kwa upande wake Dk. Nchemba alisema amefurahi kupata heshima ya kuwa mgeni rasmi katika Baraza hilo huku akiomba kuwa na mshikamano miongono mwa jamii bila kujali itikadi za dini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles