24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mgodi mpya wa Kati wa Singida Gold wazalisha kilo 49 tangu kuanzishwa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MGODi mpya wa uchimbaji dhahabu wa Kati wa Singida Gold Mine unaomilikiwa na Kampuni ya Shanta Gold Mining Company Limited uliopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida umezalisha zaidi ya kilo 49 za dhahabu tangu kuanza uzalishaji mwezi Machi, 2023.

Akizungumza katika mgodi huo, Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo amesema mgodi huo umeanza rasmi uzalishaji wa dhahabu Machi, mwaka huu ambapo zaidi ya kilo 49 za dhahabu zimezalishwa na mgodi katika kipindi cha mwezi mmoja kufikia sasa na inatarajiwa kuuzwa kwenye masoko mbalimbali hivi karibuni.

Kaimu Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo.

“Kwetu sisi uwekezaji wa mgodi wa Shanta ni muhimu sana kwenye Mkoa kwa sababu ya kuongeza maduhuli kutokana na tozo mbalimbali ambazo watakuwa wakilipa kwa mauzo ya dhahabu katika malipo ya mrabaha na ada ya ukaguzi,” alisema Mjiolojia Chone.

Aidha, wananchi wa mkoa wa huo watanufaika na mgodi wa Shanta kwa kuongeza kipato katika shughuli mbalimbali wanazozifanya kwenye maeneo ya mgodi na wale waliopata ajira kwenye mgodi.

“Mgodi wa Singida umekuwa na Sera nzuri sana ya utoaji wa ajira kwa wazawa na wakazi wa Kata ya Mang’onyi na vijiji vyake vitano vinavyozunguka mgodi huo ambapo iliundwa kamati maalumu ambayo ilikuwa inaratibu zoezi la ajira,” ameongeza Mjiolojia Chone.

Kwa upande mwingine, kutokana na ukubwa wa mgodi huo umeajiri watu wengi ambao hawakuweza kupata makazi kwenye mgodi huo na hivyo kuwanufaisha wakazi wa Mang’onyi wanaopata kipato kutokana na kupangisha nyumba kwa watumishi wa mgodi.

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa mgodi mpya wa kati wa Singida ilifanyika Oktoba 16, 2020. Mgodi wa Singida umekuwa mgodi wa pekee wa Kati kuanza uzalishaji mkoani Singida kwa kufanya uwekezaji mkubwa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya mgodi, afya na miradi mbalimbali ya maendeleo ili watanzania wanufaike ra madini hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles