Bushoke hana mpango na wasanii wapya

0
984

bushokeNA MWANDISHI WETU

MSANII aliyewahi kuwika nchini, Bushoke, amedai kwamba hana mpango wa kuwashirikisha wasanii ambao wanafanya vizuri kwa sasa ili kurudi katika ubora wake.

Bushoke amesema anaamini kuwa ana uwezo mzuri wa kuimba na kitakachomfanya arudi katika ubora wake ni uwezo wake mwenyewe na sio wasanii wanaowika kwa sasa.

“Naweza kufanya kazi na wasanii ambao wanafanya vizuri kwa sasa au zamani kutokana na aina ya msanii mwenyewe na wimbo wangu.

“Mwenyewe najiamini kuwa ninaweza kufanya vizuri kama nikiamua kurudi kwa nguvu zangu zote kwenye gemu kwa kuwa uwezo bado ninao,” alisema Bushoke.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here