Brown: Whitney amemuita mtoto wake

0
784

Bobby brownNEW YORK, MAREKANI

BABA wa marehemu Kristina Brown, Bobby Brown, amesema kuwa mama wa mtoto huyo, Whitney Houston, amemuita mwanaye ili wawe pamoja katika makazi ya milele.

Whitney alifariki tangu mwaka 2012 na kumuacha mtoto wake, Kristina, hata hivyo mtoto huyo naye alifariki Julai mwaka huu, baada ya kuugua kwa miezi sita.

Baba wa mtoto huyo, Brown, amesema kuwa Whitney amemuita mtoto wake ili waweze kukaa pamoja katika maisha ya milele.

Baada ya Kristina kufariki alizikwa karibu na kaburi la mama yake, hivyo Bobby anaamini Whitney alikuwa anamuita mtoto wake.

“Ninaamini Whitney alikuwa hana furaha kuishi peke yake huko aliko na ndiyo maana naweza kusema kuwa amemuita mtoto wake waweze kuwa pamoja, ila nawatakia wapumzike kwa amani,” alisema Brown.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here