24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Brown: Nilitaka kujiua kwa sababu ya Rihanna

Celebrities At The Lakers GameNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Chris Brown, ameweka wazi kwamba alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake, Robyn Fenty ‘Rihanna’ kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.

Alisema hayo katika maelezo mafupi aliyoyatoa msanii huyo ikiwa ni sehemu ya historia ya maisha yake ijulikanayo ‘Karibu katika maisha yangu’ huku akidai kwamba hakutegemea kuachana na mrembo huyo.

”Nilikuwa katika kilele cha muziki duniani, nyimbo zangu zikiongoza na nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui kwa umma kutokana na kumpiga Rihanna.

“Baada ya tukio hilo kuonekana kuwa kubwa nilikosa amani, nilishindwa kula na kuna wakati nilikosa usingizi kabisa, kitendo hicho kilinifanya nitamani kujiua,” aliandika Brown.

Kutokana na kitendo hicho msanii huyo alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuatia shambulio hilo. Hata hivyo, kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji mmoja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles