20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyemtoa Rose Muhando ageukia Bongo Fleva

DEEY (1)NA MWANDISHI WETU

 

PRODYUZA Ramadhani Lwambo (Deey), ameibuka na kudai kwamba baada ya midundo yake kuleta mafanikio makubwa kwa wasanii wengi kwa sasa naye ameamua kuingia katika uimbaji wa muziki wa Bongo Fleva ili aongeze chachu ya muziki huo na mashabiki wapya.

Wasanii aliowahi kuwaandalia kazi zao na nyimbo zao katika mabano ni pamoja na Christina Shusho (Unikumbuke), Flora Mbasha (Fanya Njia), Upendo Nkone (Zipo Faida), Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) na (Chapa Mwendo), Martha Mwaipaja (Usikate Tamaa) na (Nibebe) wa Rose Muhando.

Wengine ni Faraja Ntaboba (Mke wa Pili),Anastasia Mukabwa (Vua Kiatu) na hivi karibuni amerekodi albamu ya Maajabu ya ‘Damu ya Yesu’ ya George Kayala ambayo nayo kwa sasa inafanya vizuri sokoni.

“Wapo wasanii wengi maarufu nimeandaa kazi zao mimi lakini jina langu linaonekana kama ndiyo naanza kujikongoja katika muziki wakati ni mkongwe katika miziki mbalimbali ikiwemo mchiriku, muziki wa injili na Bongo Fleva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles