Miss Udzungwa kupatikana Aprili 29

MISS UDZUNGWANA ESTHER GEORGE

MSHINDI wa shindano la kumtafuta mrembo wa milima ya Udzungwa ‘Miss Udzungwa’ anatarajiwa kujishindia kitita cha shilingi 300,000.

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Flora Theophil, mshindi wa pili atapata shilingi 250,000 na watatu 150,000.

Shindano hilo limepangwa kufanyika Aprili 29 mwaka huu katika ukumbi wa Twiga Hotel uliopo mji mdogo wa Mang’ula Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro likishirikisha warembo 12.

Alisema lengo la shindano hilo ni kuitangaza hifadhi ya milima ya Udzungwa na kukuza vipaji vya warembo hao huku shindano hilo likipewa nguvu na hifadhi ya milima hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here