27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mbwa avuruga ratiba ya muziki Caribbean

Joss Stone leaving the ITV studios, LondonLONDON, ENGLAND

NYOTA wa muziki nchini Uingereza, Joss Stone, ameahirisha tamasha lake la muziki katika visiwa vya Caribbean baada ya mbwa wake kuugua.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, msanii huyo aliandika kwamba anavyoishi na mbwa wake anayejulikana kwa jina la Missy ni sawa na mtoto wake hivyo akiwa anaumwa lazima amwangalie na kumhudumia.

“Najua jambo hilo linaonekana kama la kushangaza lakini ukweli ni kwamba mbwa huyu kwangu ni kila kitu.

“Nimeamua kuvunja tamasha langu la Jumamosi katika kisiwa cha Barbados na Jumanne katika kisiwa cha Trinidad baada ya mbwa wangu kuwa mgonjwa. Nawaahidi nitarejea, lakini kwa sasa Missy yuko mbele ya mambo mengine yote,” aliandika kwenye ukurasa huo.

Msanii huyo amedai anatarajia kufanya maonyesho yake India, Nepal, Panama na Costa Rica kama sehemu ya safari yake nchi mbalimbali kuitangaza albamu yake ya saba ya ‘Water For The Soul’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles