28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

BRAZIL YASAMEHE DENI LA BIL. 445/-  KWA TANZANIA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dola za Marekani milioni 203 ambazo ni sawa na zaidi ya  Sh bilioni 445.

Deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja riba.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilieleza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dk. Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo kwa niaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dk. Sonia Portella Nunes akisaini kwa niaba ya Serikali ya Brazil.

Balozi Nchimbi alishukuru Serikali ya Brazil kwa msamaha huo ambao alisema umeunga mkono jitihada za Rais Dk. John Magufuli kujenga uchumi imara wa Tanzania.

Balozi Nchimbi pia aliihakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na Brazil.

Kiongozi wa ujumbe wa Brazil kwenye sherehe hiyo,  Guilheme Laux, Undersecretary of Credit and Guarantee kutoka Wizara ya Fedha ya Brazil alitamka rasmi kufunguliwa kwa milango ya ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na deni hilo lililofanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye madeni sugu ya Brazil.

Hivyo kutoka sasa makampuni ya Brazil yanaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania, lakini pia Serikali ya Tanzania inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles