31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KIGOGO TRA, WENZAKE KORTINI

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

SERIKALI imewafikisha mahakamani watu watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Reuben Mwakasa kwa kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 29.

Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi.

Faraja aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, mkazi wa Makongo Juu.

Akiwasomea mashtaka, Nchimbi, alidai  washtakiwa kwa pamoja walitenda makosa kati ya Novemba 22, 2013 na Agosti 21, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali Wilaya za Temeke na Ilala.

Alidai washtakiwa kwa pamoja kwa vitendo vyao waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya kiasi hicho kwa kukwepa kulipa kodi kwenye mamlaka hiyo.

 

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Nchimbi alidai upelelezi haujakamilika na kuomba kesi hiyo kuahirishwa hadi tarehe nyingine kwa kutajwa.

Washtakiwa walipelekwa rumande na kesi imepangwa kutajwa Septemba 27, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles