27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bosphorus yatambulisha sokoni bidhaa za ujenzi za Yapfix

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

BIDHAA za Yapfix zinazotengeza na kiwanda cha Bosphorus maalum kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zimetambulishwa rasmi sokoni huku uwekezaji wake ukigharimu takribani Sh bilioni mbili.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa kiwanda hicho, Alex Kaaya alisema bidhaa ya Wally Putty nayo inafanya vizuri sokoni kutokana na ubora wa kiwango cha juu unaotumika katika uzalishaji.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Necmetin Keles, akionyesha malighafi za mawe wanazotumia kuzalisha Gundi Yapfix mbayo ni maalum kubandikia vigae (tiles) ukutani na sakafuni kwenye nyumba ambayo ina uwezo mkubwa wa kuizuia unyevunyevu unaosababishwa na maji ukutani, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna viwanda vingi vinazalisha bidhaa kama hizo, lakini hazina ubora kama tunazozalisha kwenye kiwanda chetu.

“Bosphorus tuna Wally Putty yetu ya kipekee ambayo hairuhusu maji kuingia kwenye ukuta na kutengeneza unyevu, inatengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya kutoka Uturuki, nyingine inazuia fangasi kwenye ukuta”alisema.

Naye Mkurugenzi  wa kiwanda hicho, Necmetin Keles alisema tangu wameanza mwaka 2015 wameajiri wafanyakazi 35 na kadiri watakavyojipanua wanakusudia kuongeza ajira nyingine.

Alisema asilimia kubwa ya malighafi zinazotumika zinatoka hapa nchini, akitolea mfano wa mawe na mchanga utoka kwa wafanyabiashara wadogo ambao nao wananufaika.

Alitaja bidhaa nyingine zinazozalishwa na kiwanda hicho ni za mapambo (decorative plaster), gundi maalum za kubandika vigae na nyingine nyingi zenye ubora wa hali ya juu.

BIDHAA za Yapfix zinazotengeza na kiwanda cha Bosphorus maalum kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zimetambulishwa rasmi sokoni huku uwekezaji wake ukigharimu takribani Sh bilioni mbili.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa kiwanda hicho, Alex Kaaya alisema bidhaa ya Wally Putty nayo inafanya vizuri sokoni kutokana na ubora wa kiwango cha juu unaotumika katika uzalishaji.

Alisema kuna viwanda vingi vinazalisha bidhaa kama hizo, lakini hazina ubora kama tunazozalisha kwenye kiwanda chetu.

“Bosphorus tuna Wally Putty yetu ya kipekee ambayo hairuhusu maji kuingia kwenye ukuta na kutengeneza unyevu, inatengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya kutoka Uturuki, nyingine inazuia fangasi kwenye ukuta”alisema.

Naye Mkurugenzi  wa kiwanda hicho, Necmetin Keles alisema tangu wameanza mwaka 2015 wameajiri wafanyakazi 35 na kadiri watakavyojipanua wanakusudia kuongeza ajira nyingine.

Alisema asilimia kubwa ya malighafi zinazotumika zinatoka hapa nchini, akitolea mfano wa mawe na mchanga utoka kwa wafanyabiashara wadogo ambao nao wananufaika.

Alitaja bidhaa nyingine zinazozalishwa na kiwanda hicho ni za mapambo (decorative plaster), gundi maalum za kubandika vigae na nyingine nyingi zenye ubora wa hali ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles