24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aishukuru Marekani, yampa tano kwenye Demokrasia

Na Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameishukuru Marekani kwa msaada katika Sekta mbalimbali ikiwemo afya ambapo amesema kupitia misaada yao ukiwemo Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Ukombozi wa UKIMWI (PEPFAR) kwa sasa UKIMWI na hata Kifua Kikuu havitishii tena maisha ya Watanzania na maambukizi ya UKIMWI yameshuka kutoka 7.2% mwaka 2012 hadi 4.7% mwaka 2016/2017 na umepungua zaidi mwaka 2021.

Akiongea Ikulu Dar es Salaam leo mbele ya Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani, Kamalla Haris, Rais Samia amesema

“Tunaishukuru Marekani kwa msaada katika Sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, chakula, demokrasia, haki za Binadamu na utawala bora, kwa mfano katika Sekta ya Afya UKIMWI na Kifua Kikuu havitishii tena maisha ya Watu wetu, maambukizi ya UKIMWI yameshuka kutoka 7.2% mwaka 2012 hadi 4.7% mwaka 2016/2017 lakini umepungua zaidi mwaka 2021.

“Maambukizi ya mapya ya kifua kikuu yamepungua kutoka Watu 306 kati ya kila Watu Laki 1 hadi Watu 208 kwa kila Watu Laki 1, Wanawake Wajawazito wenye virusi vya UKIMWI sasa wana uhakika wa kuzaa Watoto wasio na UKIMWI na hizi ni jitihada za PEPFAR tunawashukuru sana.

“Kupitia msaada wenu Marekani, vifo vya Malaria vimepungua sana kutoka Milioni 7. 7 mwaka 2015 hadi Milioni 3.5 kwahiyo tumepunguza kwa zaidi ya nusu na nadhani kwa jitihada zaidi tutapunguza kabisa na lengo letu ni kuwa na Taifa lisilo na Malaria kabisa, tupo tayari kumpokea Mwekezaji yoyote anayetaka kuanzisha kiwanda cha dawa Tanzania na hii ni kwasababau tunataka kupunguza mnyororo wa thamani, tukizalisha dawa Tanzania gharama zitakuwa ndogo,” amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles