24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani kuipa Tanzania Dola milioni 560 mwaka 2024

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali ya Marekani imesema inakusudia kutoa Dola za Kimarekani milioni 560 kama msaada rasmi kwa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2024 hii ikiwa ni katika kusaidia kuongeza wigo na kina cha uhusiano rasmi kati ya nchi hizo mbili.

Makamu wa Rais Harris wa Marekani ametangaza ahadi hiyo leo Machi 30, Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo ametangaza pia miradi mingine ya kuimarisha ubia kati ya Marekani na Tanzania.

“Ubia kati ya Marekani na Tanzania umekita mizizi katika zaidi ya miongo sita ya ushirikiano katika nyanja za uchumi, maendeleo, afya na usalama, Marekani na Tanzania zinasimama pamoja kama Marafiki na Wabia, kwa kuzingatia misingi ya kuheshimiana na malengo ya pamoja ya kuwa na mustakabali wenye amani na ustawi zaidi.

“Marekani inaunga mkono kikamilifu ajenda ya Tanzania ya mageuzi ya kidemokrasia na ina dhamira thabiti ya kusaidia kuendeleza maadili ya kidemokrasia ya Tanzania, ziara yangu nchini Tanzania inathibitisha ubia huu imara baina ya Nchi zetu mbili na itaimarisha zaidi ushirikiano katika biashara, jitihada za kutafuta ufumbuzi kuhusu usalama na uhakika wa chakula, ulinzi wa bayoanuai za majini, uwekezaji kwa Wanawake na Vija, afya na kuimarisha demokrasia,” amesema Harris.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles