28.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

BODI YA SUKARI YATAKA UZALISHAJI UWE TANI 420,000

Na RAMADHANI LIBENANGA,-MOROGORO


BODI ya Sukari imewataka wamiliki wa viwanda vya sukari kuweka mipango madhubuti ya kupanua uwezo wa uzalishaji sukari nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari, Andrew Semweza, wakati wa  uzinduzi wa kamati ya uhamasishaji wa kubadili mfumo wa uendeshaji  wa umoja wa wakulima wa miwa katika Bonde la Mto Kilombero, kutoka katika vyama vya kijamii  kwenda mfumo wa ushirika.

Katika uzinduzi huo uliofanyikia wilayani Kilombero, Semwenza alisema viwanda vya sukari vinapaswa kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuzalisha tani 420,000 za sukari ifikapo mwaka 2020.

Alisema kampuni zinazosimamia viwanda hivyo zinapaswa kutoa ushirikiano na kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo cha miwa.

Naye kiongozi wa chama cha wakulima wa miwa Kidatu, Bakari Mkangamo, alisema  mabadiliko yanafanyika, lakini baadhi ya wananchi hawako tayari kukubali mfumo mpya kwa sababu umekuja ghafla na hawajui faida yake.

Mabadiliko ya kutoka vyama vya kijamii vya wakulima wa miwa na kuingia mfumo wa ushirika yanafanyika chini ya Sheria ya Sukari ya mwaka 2011, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015, inayomtaka mkulima kujiunga na ushirika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles