30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

BLAC CHYNA ‘AMBWAGA’ YBN ALMIGHTY JAY

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa mitindo nchini Marekani, Blac Chyna, amethibitisha kuachana na mpenzi wake, YBN Almighty Jay, baada ya kusema kuwa yupo singo kwa sasa.

Blac mwenye umri wa miaka 30, alikuwa kwenye uhusiano na kijana huyo mwenye umri wa miaka 18, mara baada ya mrembo huyo kuachana na baba wa mtoto wake Rob Kardashian.

Mrembo huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuthibitisha kuwa hayupo kwenye uhusiano na hana mpango wa kufanya hivyo kwa sasa.

“Kwa sasa sipo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote, nataka watu wajue hilo na sina mpango kwa kipindi cha hivi karibuni,” aliandika mrembo huyo.

Blac ni mama wa watoto wawili, kabla ya kupata mtoto wa pili na Rob, tayari alikuwa amefanikiwa kupata mtoto na rapa Tyga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles