23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

AMBER ROSE AKANUSHA KUTOKA NA LIL PUMP

WIKI iliyopita picha ya mrembo, Amber Rose na rapa Gazzy Garcia maarufu kwa jina la Lil Pump, zilileta mjadala kuwa wawili hao wapo kwenye uhusiano, lakini mrembo huyo amekanusha taarifa hizo.

Picha hiyo ilikuwa inamuonesha Amber Rose akimwashia sigara rapa huyo huku ikiwa mdomoni, hivyo ilileta mjadala mkubwa kwa mashabiki zao ambao walidai kuwa wawili hao wameanzisha uhusiano.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Amber Rose aliweka wazi kuwa Lil Pump ni mtoto mdogo sana na ni kama mtoto wake, hivyo hawezi kuwa kwenye uhusiano na rapa huyo.

“Lil Pump ana umri wa miaka 17, ni mdogo sana kwangu, nimemwacha miaka 17, hivyo siwezi kuwa naye kwenye uhusiano ana uwezo wa kuniita mama.

“Sitaki kusikia habari hizo, kumwashia sigara haiwezi kuwa sababu ya kuwa kwenye uhusiano na kijana huyo kama watu wanavyodhani,” aliandika mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles