30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

NIKKI BELLA, JOHN CENA WARUDIANA

CALIFORNIA, MAREKANI


HATIMAYE mwanamitindo Nikki Bella na mkali wa mchezo wa mieleka, John Cena, wamemaliza tofauti zao na kurudiana baada ya kudaiwa kuachana.

Wawili hao ambao walitangaza kuwa wapo kwenye mipango ya kufunga ndoa, walidaiwa kuachana mapema mwezi uliopita, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita walionekana wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza.

Mastaa hao walionekana wakiwa wanaelekea kunywa kahawa kwenye Mji wa San Diego huko California. Hata hivyo, Cena alifunguka na kusema kila kitu kipo sawa.

“Bado ninampenda Nikki, bado nina lengo la kutaka kufunga ndoa na Nikki, bado ninatarajia kuwa na familia na Nikki,” alisema staa huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles