25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Bina: Wachimbaji wadogo njooni tujenge hoja kwa Serikali

Clara Matimo, Mwanza

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania(FEMATA, John Bina, amewaasa wachimbaji kuhudhuria kwa wingi kwenye kongamano la wachimbaji wadogo wa madini litakalofanyika jijini Mwanza Mei 9, 2023 ili kujenga hoja kwa serikali zitakazowawezesha kuendeleza sekta ya uchimbaji madini.

Bina amesema mgeni rasmi katika kongamano hilo atakuwa ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, hivyo ni vyema wachimbaji hao wakatumia fursa hiyo kueleza changamoto wanazokabiliana nazo na kutoa suluhisho kwa serikali nini kifanyike ili malengo ya FEMATA yaweze kutimia ikiwemo kuwa na siku ya madini kitaifa pamoja na benki ya madini.

“FEMATA tunaamini hayo malengo yetu yakitimia tutaweza kuwasaidia wachimbaji wetu na uchimbaji utatunufaisha tunahitaji tumuonyeshe Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa kwamba wale wachimbaji wadogo wa leo sio wale wa zamani, wachimbaji wa sasa tunafikilia kuwa wachimbaji wa kati na wakubwa.

“Hivyo, lazima tuonyeshe uwezo wa kufikiri na kujenga hoja, imani yetu ni kwamba Waziri Mkuu atazibeba hoja zetu na kuzitolea majibu na mimi kama kiongozi wa wachimbaji wadogo wa madini hapa nchini ninaimani sana na Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa,” amesema Bina na kuongeza:

“Tunahitaji kutoa hoja ambazo zitaifanya dunia ijue kwamba wachimbaji wadogo wa Tanzania wametosha kuchimba madini na wanahitaji sapoti, kuna vitu vingi kama ruzuku tunahitaji kuihakikishia serikali ili itambue kwamba ikitupa ruzuka itafanya kazi ambayo imelengwa na hiyo ruzuku yenyewe,” amesema.

Katika hatua nyingine, Bina amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi kupitia kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo ya kimkakati na kuimarisha ushirikiano na nchi za nje hali inayowafanya wapate fursa nyingi katika sekta hiyo.

Aidha, amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kukubali kuwasikiliza wadau wote wa sekta ya madini kupitia kongamano hilo ambapo pia aliipongeza Wizara ya Madini inayoongozwa na Dk. Doto Biteko kwani imekuwa mstari wa mbele kuwasilikiza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi mapema.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania(TAWOMA), Semeni Malale, amewahamasisha wanawake wote katika sekta hiyo kuhudhuria kongamano hilo kwani ni fursa na nafasi ya kipekee kwao kuwasilisha changamoto zao kwas erikali kupitia kwa Waziri Mkuu Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles