25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kiruswa  kutembelea mabanda  ya maonesho wiki ya madini

Na Clara Matimo, Mwanza

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Dk. Steven Kiruswa Mei 8, 2023 anatarajia kutembelea mabanda mbalimbali  yaliyopo kwenye maonesha ya WIKI YA MADINI inayofanyika katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Wiki ya Madini, Kongamano la Wachimbaji na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) 2023, Solomon Mabati alipozungumza na MTANZANIA DIGITAL Mei 7, 2023 katika viwanja vya Rock City Mall kuhusu maendeleo ya maonesho hayo.

Mabati amesema Dk. Kiruswa atapata fursa ya kuona teknolojia za kisasa za uchimbaji madini, ambazo wachimbaji wadogo wamekuwa wakizitumia hivyo kuwasaidia kufanya uchimbaji wenye tija.

“Miaka ya nyuma wachimbaji tulikuwa tunatumia zana duni kwa ajili ya kuchimba madini lakini sasa tumepanda kiwango tunatumia teknolojia za kisasa ambazo baadhi ziko hapa kwenye maonesho haya ya wiki ya madini.

“Tunaishukuru sana serikali yetu kupitia Wizara ya Madini  kwa kuendelea kutulea sisi wachimbaji wadogo, kwetu sisi FEMATA ujio wa viongozi hao ni fursa kubwa sana kwani tunaamini hata ushauri au maelekezo watakayoyatoa tutayafanyia kazi,” amesema Mabati na kuongeza

“Tumekuwa   tukishirikiana na serikali siku zote ili kuhakikisha tunanufaika na rasilimali madini zilizopo katika nchi yetu sisi wenyewe, familia zetu, jamii na taifa kwa ujumla,” ameeleza Mabati.

Wiki ya madini ilizinduliwa Mei 4, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima ikiwa imeambatana na mambo  tofauti tofauti ikiwemo maonesho ya teknolojia za kisasa za uchimbaji madini, elimu ya mikopo ya uchimbaji kutoka taasisi za fedha na elimu ya afya kwa ajili ya kutunza afya na mazingira nchini.  

Maadhimisho hayo yanaongozwa na kauli mbiu  isemayo  ‘Amani iliyopo Tanzania Itumike Kuwa Fursa ya Kiuchumi na Tanzania kuwa Kitovu cha Biashara ya Madini Afrika’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles