23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatambulisha mfumo mpya wa uagizaji dawa Mwanza

Na Clara Matimo, Mwanza

Serikali imetambulisha mfumo mpya wa mshitiri mkoani Mwanza ukakaosaidia katika uagizaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi, zinazokosekana katika Bohari la Dawa.

Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dk.Thomas Rutachunzibwa.

Hayo yemeelezwa Mei 6, 2023 na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa huo, Claudia Kaluli alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kuhusu namna ya kutumia mfumo huo kwa wakurugenzi kutoka katika Halmashauri zote zilizopo mkoani humo, waganga wakuu wa wilaya, maafisa TEHAMA, waratibu wa huduma za maabara na Maafisa ugavi.

“Wizara ya Afya ikishirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeleta mfumo ya uagizaji dawa ujulikanao kama mfumo wa mshitiri ambazo zitakuwa zinakosena katika Bohari la Dawa ambao ni rahisi na utasaidia kuweza kushirikiana na wauzaji binafsi,” mesema Kaluli.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Balandya Elikana alisema Serikali inaendelea kuimarisha njia za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi mkoani humo ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi zinatolewa kwenye vituo vya afya nchi nzima.

Elikana ameipongeza TAMISEMI ambao ndiyo wawezeshaji wa mafunzo hayo kwa kuendelea kuboresha mfumo wa mshitiri kwani endapo utasimamiwa vizuri utasadia upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

“Niipongeze TAMISEMI kwa kuendelea kuboresha mfumo wa mshitiri ni matumaini yangu na Serikali kuwa mfumo huu endapo utasimamiwa vizuri utasaidia katika upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, zinazokosekana katika Bohari la Dawa kwa urahisi na haraka,” amesema Elikana.

Mratibu wa Huduma za Maabara na Damu Salama Mkoa wa Mwanza, Julius Shigella, alisema anaamini mfumo huo utaleta mageuzi chanya kwenye sekta ya afya kutokana na upatikanaji wa haraka wa dawa na usahihi wa nyaraka husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles