23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Lindi Mwambao wapongezwa kwa usimamizi mzuri wa uuzaji mazao

Na Hdija Omary, Lindi

MKUU wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga ameipongeza bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Lindi mwambao kinachojumuisha wakulima wa Halmashauri za Kilwa, Mtama na Lindi Manispaa kwa kusimamia vizuri uuzaji wa zao la korosho katika misimu miwili iliyopita 2021/2022 na 2022/2023.

Ndemanga ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wanaushirika kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katika mkutano mkuu wa sita wa mwaka 2023 wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Nyangao Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi.

Ndemanga amesema licha ya changamoto ambazo zimejitokeza katika baadhi ya maeneo lakini kwa kiasi kikubwa wameweza kuondoa malalamiko hasa yanayohusiana na malipo kwa wakulima.

“Ilifika mahala mpaka nilisahau kama msimu wa korosho unaendelea, sikupata shida yoyote kwenye chama chochote hii inamaana kwamba sasa viongozi mnajua majukumu yenu mnauwezo wa kusimamia na kuwasaidia wakulima wenu hongereni sana,” amesema Ndemanga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai amewasisitiza viongozi  wa bodi kuendelea kuvisimamia ipasavyo vyama vyao vya msingi (AMCOS) ili mali za wanaushirika ziweze kuleta maendeleo na kuvifanya vyama hivyo kuwa endelevu  na kuaminika na wadau wake.

“Kama bodi itasimamia vizuri vyama vya msingi, vyama vyenu vita aminika na wanachama pamoja na wakulima kwani wapo baadhi ya watu wanauchukia ushirika kutokana na mambo mahovu yanayofanywa na baadhi ya viongozi waliomo,” amesema Ngubiagai.

Nae, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Lindi, Secilia Sostenes amesema pamoja usimamizi mzuri unaoendelea kufanywa na bodi katika mauzo, bodi ya chama hicho pia inatakiwa kusimamia vyama vya msingi ( AMCOS) viweze kujiendesha kwa kuanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo.

Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji wa chama, Mwenyekiti wa chama hicho, Ismail Nalinga amesema wao kwa kushirikiana na kamati ya Elimu na Mafunzo ya Mkoa kimejiwekea utaratibu wa kuendelea kutoa mafunzo kwa watumishi pamoja na nawachama wake kabla ya mkutano mkuu wa kawaida wa mwaka na msimu wa mauzo ya mazao kuanza kwa lengo la kuwajengea uwezo wa utoaji wa huduma kwa wanachama wao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles