Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam
Serikali imetenga Sh bilioni tisa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa fukwe ya kisasa ya Coco (Coco beach).
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema mradi huo utakaoanza hivi karibuni utaiweka katika mandhari nzuri fukwe hiyo na kutoa fursa kwa Watanzania kufika kwenye maeneo hayo kupunga upepo.
“Serikali imeamua kulibadilisha Jiji la Dar es Salaam liwe la kisasa na la kibiashara, jambo ambalo limesababiaha fukwe ya Coco kurudishwa serikalini ili iweze kutumiwa na wananchi wote,” amesema Makonda.
Amesema licha ya kuwapo kwa miradi mingine ya uboreshaji wa jiji kuanzia kwenye makazi ya watu hadi miundo mbinu ya barabara ili iweze kufikika kwa urahisi.