27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

SPIKA: TUWAOMBE WENYE MAMLAKA MAWAZIRI WASAFIRI

Gabriel Mushi, Dodoma

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuna haja ya wabunge kuwaombea mawaziri kwenye mamlaka husika ili wapate fursa kusafiri nje ya nchi.

Kau;I hiyo ya Spika Ndugai imeungana na baadhi ya hoja za Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo), wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Katika mchango wake Zitto alisema ni muhimu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage asafiri nje ya nchi, ili kujenga uhusiano ya kidiplomasia na kutafuta masoko ya bidhaa za mbaazi, choroko na giligilani.

Kutokana na kauli hiyo, Spika Ndugai amekiri kuguswa na mchango huo na kusisitiza kuwa ni kweli mawaziri inabidi wasafiri.

“Waziri wa Biashara hawezi kukaa na sisi hapa, lazima ende, tumuombee popote pale kwenye mamlaka lazima asafiri, maana bidhaa zetu tutauza Kongwa, kuna soko huko?

“Waziri wa utalii lazima asafiri ‘apige mawingu’ huko na wengine huko, ndiyo ukweli jamani, sisi wabunge lazima tuwasemee,” amesisitiza Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles