23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni  7/- kununua dawa za saratani

samia-suluhuNA MASYENENE DAMIAN

SERIKALI imesema mapambano dhidi ya magonjwa ya wanawake hususan saratani ya shingo ya kizazi na matiti yamewekewa kipaumbele.

Kipaumbele hicho ni pamoja na kununua dawa za saratani, kupunguza bei ya dawa hizo na kuendeleza huduma za upimaji wa awali wa dalili za magonjwa hayo ili kuwafikia wanawake wengi zaidi.

Hayo yameleezwa   Mwanza   na Makamu wa Rais wa Tanzania, SAMIA SULUHU katika uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi.

Alisema   azma ya serikali ni kuboresha afya ya mama, msichana na mtoto na kutoa elimu kwa wananchi  waweze kutambua athari za saratani hizo wajenge tabia ya kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara.

Suluhu alisema serikali katika mwaka wa fedha 2016/17 imetenga Sh bilioni saba kwa ajili ya kununulia dawa za saratani kutoka Sh bilioni moja ya mwaka jana.

Alisema  jitihada znaifanyika kupunguza gharama za dawa za saratani ambazo hivi sasa ni Sh 200, 000  hadi Sh 300, 000 kwa pakiti moja ya dawa.

“Serikali tunatambua changamoto hizi na tayari tumeshaweka mipango thabiti ya kukabiliana na kutokomeza  saratani.

Tutashirikiana  na wadau  kuzifanya huduma za uchunguzi ziwe endelevu katika kutekeleza azma yetu hii.

“Tayari Wizara ya Afya imeshapokea Sh. Bilioni tano kutoka Benki ya Dunia ili kuwa na vituo vitatu katika kila hamashauri kuboresha shughuli za uchunguzi na matibabu ya mapema   wanawake kote nchini waweze kuzipata huduma hizi kwa urahisi,”alisema.

Alisema  serikali pia inalenga kuanzisha huduma za matibabu ya mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na KCMC   kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaosubiri matibabu ya saratani Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam.

“Wagonjwa wengi hufika hospitalini wakiwa katika hatua ambayo saratani hiyo haiwezi kutibika tena hivyo kufanya takwimu za vifo vya saratani hiyo kuzidi kupaa.

“Kwa pamoja, saratani ya mlango wa kikazi na matiti husababisha zaidi ya asilimia 60 ya vifo vyote vya kina mama,” alisema.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kuna changamoto nyingi zinazosababisha kina mama wengi kutogundulika mapema na hatimaye kufariki dunia kabla ya kupata huduma.

“Uelewa mdogo, imani potofu, gharama kubwa za matibabu, unyanyapaa na kuwapo  vituo vichache vya kufanya uchunguzi wa kutoa tiba ya mionzi,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles