22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Waathirika tetemeko la wapewa mabati, saruji

waathirika-tetemekoNa  Renatha Kipaka

MAKUNDI ya wasiojiweza ambao ni waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera wameanza kupatiwa msaada wa  mabati 20 kwa kila kaya na mifuko mitano ya ya saruji.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa  wananchi hao katika wilaya sita za mkoa huo kwa kuanza na wazee, walemavu, wajane na watu wasiojiweza.

Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali mstaafu, Saalim Kijuu alifanya uzinduzi juzi wa ugawaji wa vifaa hivyo katika   ofisi ya Kata ya Kashai katika Manispaa ya Bukoba.

Alisema   vifaa vya ujenzi kwa makundi hayo utafanyika katika  wilaya za Muleba, Misesenyi,Karagwe,  Manipaa  ya Bukoba na Bukoba Vijijini.

Alisema  hatua ya awali imegawa kaya 200 kati ya kaya 370 kwa kuanzia  mtaa wa Rwome na   Kijiji cha Ibosa katika kata ya Nyakato.

Aneth Kiiza, mkazi wa mtaa wa  Rwome Kata Kashai akizungunza kwa niaba ya mama yake imelda Kiiza (95), alisema aliwashukuru  viongozi kwa msaada huo.

Alisema  nyumba aliyokuwa akiishi mama huyo ilianguka ukuta  upande wa kulia na kushoto na walikosa maeneo ya kuishi kwa muda mrefu.

Kiiza alisema misaada aliyopewa mama yake itasaidia kupata angalau chumba kimoja cha kuishi.

Alisema mama yake  hana uwezo wa kujijengea   nyumba kutokana na hali yake ya uchumi kuwa duni.

Pia alisema kuwa gharama za ujenzi wa nyumba nzima ni Sh milioni  4.8, fedha ambazo hana.

Diwani wa Kata ya Kashai,  Nurulhuda Kabaju (Chadema),  alisema   yanapotokea matatizo kama ya tetemeko la ardhi watoto wawakumbuke wazazi wao kwa kutoa misaada ya  hali na mali.

Khafisa Khamis (75) mkazi wa Kijiji cha Ibosa Kata Nyakato ambaye ni mjane alisema nyumba yake  ilipasuka  kila kona hivyo anaishukuru  serikali kwa kumpatia mifuko mitano ya saruji   na mabati 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles