26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri atoa maagizo mazito Mwauwasa

gerson-lwengeNa BENJAMIN MASESE

WAZIRI wa  Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge,  ametoa maagizo mazito kwa bodi mpya ya  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mwanza (MWAUWASA).

Ameitaka kuhakikisha inapanua mtandao wa kuwapatia wananchi huduma ya maji safi, majitaka na kupunguza upotevu wa maji unaofikia asilimia 37.

Pia ameziondolea halmashauri mbili za Ukerewe na Sengerema mamlaka ya kusimamia na kukusanya mapato ya  miradi mikubwa ya maji.

Amesema  badala yake Mwauwasa ndiyo itakayohusika moja kwa moja huku akisema kwamba uzoefu na historia za halamshauri nyingi  nchini unaonyesha kutokuwa na usimamizi mzuri unaosababisha miradi kutokuwa endelevu.

Kauli hiyo aliitoa   Mwanza wakati akizindua bodi mpya ya Mwauwasa ambayo itakuwa madarakani kwa miaka mitatu (2016/2019).

Alisema bodi hiyo ina jukumu la kuongeza kasi ya utoaji huduma ya majisafi kutoka asilimia 90 ya sasa na kufikia 95 ifikapo mwaka 2025.

Lwenge   ifikapo mwaka 2020 Mwauwasa inapaswa kuwa imepiga hatua ya kusambaza miundombinu ya majitaka kutoka asilimia 25 ya sasa na kufikia 30.

Alieleza kusikitishwa na kiwango  cha upotevu wa majisafi  ambacho ni  asilimia 37.

“Bodi hii ionyesha mabadiliko makubwa, kwanza iboreshe mishahara ya watumishi kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kazi.

“Ni ukweli usiopingika Mwauwasa inafanya vizuri sana  ndiyo maana kama wizara tumeamua  kuikabidhi miradi mikubwa ya Nansio na Sengerema kuisimamia hadi kukusanya mapato, miradi  mingine inayokuja ikikamilika tutaendelea kuiweka chini yao,” alisema.

Aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutengeneza vyoo vya plastiki na mvua inaponyesha humwaga kinyesi kuelekea Ziwa Victoria jambo ambalo ni hatari  sana kwa usalama wa jamii inayotumia maji hayo.

Akiwasilisha malalamiko kwa waziri huyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Bugarika Bendera tatu, Daniel Andrew alisema licha ya mradi kuwapo hapo,   mashine inayosukuma maji imekuwa ikizimika mara kwa mara.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo, Mkurugenzi wa Mwauwasa,   Antony Sanga alisema  mradi huo ni miongoni mwa miradi ya  dharura iliyoanzishwa kwa lengo la kupeleka maji sehemu zilizokuwa muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles