FLORENCE SANAWA, LINDI
Shirika la viwango Tanzania (TBS), limesema kuwa wajasiliamali wengi Katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanazalisha bidhaa ambazo hazikidhi vigezo vya kupata alama ya ubora.
Akizungumza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kusini yanayofanyika katika viwanja vya ngongo mkoani Lindi, Ofisa Mkaguzi TBS, Dina Lweno, alisema kuwa bidhaa hizo pia zimekuwa zikizalishwa katika maeneo ambayo hayana viwango na kwamba kitendo cha kufanyia kazi Katika mazingira yasiyofaa imepelekea kusiwepo na mjasiriamali yeyote kuwa na alama hiyo kwa Mkoa wa Mtwara.
“Tunaona SIDO inajitahidi ila bado hawana maeneo mazingira bado ni duni ni vigumu kuwapa alama za ubora kuna wakati unapita kwa mjasiriamali unakuta anatwanga Karanga kwenye kinu alafu anataka alama ya ubora hili ni tatizo kubwa”alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Sebastian Waryuba, alisema kuwa bidhaa nyingi zinazozalishwa na wajasiliamali wadogo hazina uthibitisho wa TBS.
“Endapo bidhaa zikipata alama ya ubora bidhaa zetu zinaweza kuongezeka thamani kwakuwa watakuwa na uwezo wa kukuza Soko la bidhaa za ndani” alisema Waryuba