24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Brela yatumia maonyesho ya nanenane kutoa leseni za Biashara

Derick Milton, Simiyu

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela), imetumia maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, kutoa leseni za biashara daraja A kwa wasafirishaji wa mazao na mifugo nje ya nchi.

Mbali na hilo Brela inatumia maonyesho hayo kutoa elimu kwa wakulima na wafanyabiashara namna ya kupata huduma ya leseni za biashara, leseni za viwanda, kujua utaratibu wa kufanya biashara za kimataifa, usajili wa makampuni, majina ya biashara na alama za biashara.

Ofisa kitengo cha miliki bunifu wa Brela Suzana Senzo, amesema kuwa wanawajibika kushiriki kwenye maonyesho hayo hasa kufuatia kauli mbiu ya mwaka huu ya nane nane ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.

Naye Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Emmanuel Kakwezi, amesema kuwa lazima Brela ihakikishe wakulima na wafanyabiashara wanarasimisha biashara zao ili kuweza kukidhi vigezo vya soko la ndani la bidhaa zao, lakini zaidi soko la nje ya nchi ambako kuna fursa nyingi zaidi.

“Kwa sasa tunaanda mfumo unaotoa taarifa za kibiashara nchini, mfumo huu unawasaidia wafanyabishara kujua lini wanatakiwa kuuza, wapi wapate soko pamoja na vibali na mfumo huu unajulikana kama Trade Facilitation information module,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles