25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji aitaka mahakama imuhukumu AG

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

Sakata la Askofu, Mulilege Kameka, anayeshikiliwa mahabusu kwa zaidi ya miezi tisa kwa tuhuma za kutokuwa raia wa Tanzania, limechukua sura mpya baada ya yeye kuiomba mahakama hiyo iwatie hatiani Mwanasheria Mkuu wa Serikali Adelardus Kilangi na Kamishna wa Uhamiaji. #MtanzaniaDigital

Kameka ambaye ni Askofu wa Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship (HPSFCFC), ameitaka mahakama hiyo iwahukumu kifungo Mwanasheria huyo Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kwa kudharau amri ya mahakama.

Maombi hayo yaliyofunguliwa Julai 16 mwaka huu, yalipangwa kusikilizwa jana Jumatatu Agosti 5, na Jaji Atuganile Ngwala hata hivyo upande wa Serikali ambao ni wajibu maombi hayo waliwasilisha pingamizi la awali dhidi ya maombi hayo.

Baada ya pingamizi hilo Mahakama hiyo imepanga Agosti 9, mwaka huu, kutoa uamuzi juu ya pingamizi lililowasilishwa na Upande wa serikali dhidi ya maombi ya Askofu huyo.

Uamuzi huo wa Mahakama unatarajiwa kutolewa na Jaji Ngwala, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kuhususiana na pingamizi hilo lililowasilishwa na wajibu maombi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles