24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Shamte azitaka nchi za SADC kuondoa vikwazo

Nora Damian -Dar es salaam

MWENYEKITI mpya wa Baraza la Biashara katika Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Salum Shamte, amezitaka nchi wanachama kuondoa vikwazo vya kibiashara kuiwezesha sekta binafsi kutimiza majukumu yake.

Shamte ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), alikabidhiwa uenyekiti wa baraza hilo jana kutoka kwa Charity Mwiya wa Namibia aliyemaliza muda wake.

Akizungumza jana, Shamte alisema zaidi ya asilimia 90 ya ajira zinatengenezwa na sekta binafsi katika nchi za SADC, lakini bado inakabiliwa na changamoto nyingi.

“Sekta binafsi inakabiliwa na changamoto nyingi katika kufanya biashara, tunatakiwa tushirikiane na sekta ya umma kufanya kazi pamoja kuondoa vikwazo vya kikodi na visivyo vya kikodi,” alisema Shamte.

Kwa mujibu wa Shamte, kutokana na vikwazo hivyo, gharama za kufanya biashara Afrika ni zaidi ya mara saba kulinganisha na nchi za Asia.

Alisema pia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 30 zimekuwa zikitumika kuagiza chakula nje wakati kuna asilimia 60 ya ardhi inayoweza kutumika kuzalisha.

Alizitaka nchi wanachama wa SADC kuachana na ushindani usio na maana na kukumbatia zaidi ushirikiano kuhakikisha miradi midogo na mikubwa inafanikiwa.

Hata hivyo, alisema mazingira ya kibiashara hapa nchini yamekuwa yakiimarika zaidi kutokana na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali hasa katika kuboresha miundombinu.

“Tuna imani mwongozo wa maendeleo ya biashara ukianza kutekelezwa utawezesha wafanyabiashara kufanya biashara katika mazingira rafiki,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles