24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bemba kuhukumiwa miaka 25 gerezani

Jean-Pierre BembaTHE HAGUE, UHOLANZI

MAJAJI wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kesho huenda wakatoa hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela kwa mbabe wa zamani wa vita wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC),  Jean-Pierre Bemba.

Kama majaji watakubaliana na upande wa mashitaka, hukumu hiyo itakuwa ya kwanza ya kifungo cha muda mrefu gerezani kutolewa na ICC katika kesi ambayo kwa mara ya kwanza imelenga ubakaji kama silaha ya vita.

Waendesha mashitaka wanamlaumu makamu huyo wa rais wa zamani wa DRC kwa kufumbia macho vitendo viovu vilivyofanywa na vikosi vyake katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika Kati (CAR) kuanzia Oktoba 2002 hadi Mei 2003.

Alipatikana na hatia Machi mwaka huu ikihusisha mashitaka matano ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, baada ya kupeleka wapiganaji wake 1,500 CAR katika jitihada za kuzima mapinduzi dhidi ya mtawala wa wakati huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles