28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Beach Soccer yaahidi kupigania kombe COSAFA

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni ‘Beach Soccer’, inatarajia kurusha karata yake kesho Novemba 18,2021 dhidi ya Msumbiji katika michuano ya COSAFA, huku ikiahidi kupambana ili kuwapa raha Watanzania.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Kocha Msaidizi wa kikosi cha Beach Soccer, Deo Lucas, amesema timu ya soka la ufukweni imekuwa ikijitahidi kwani ndani ya miaka saba tangu kuanzishwa imeshiriki AFCON mara mbili mfululizo.

Ameeleza kuwa hata katika viwango kwa Afrika, Tanzania inashika namba saba na duniani wa 42.

“Nawaomba Watanzania wazidi kutoa sapoti katika mchezo mchezo huu, umekuwa ukiwakilisha nchi vizuri katika michuano mbalimbali,” amesema.

Kuhusu mashindano ya COSAFA amesema ndiyo yanafanyika kwa mara ya kwanza na Tanzania inashiriki kama timu alikwa.

“Lengo letu la kwanza katika mashindano haya ni kufika nusu fainali na baadaye fainali, tuna imani na wachezaji wetu kwa wiki mbili za mazoezi, pia tumewachukua katika timu zinazoshiriki Ligi ya Beach Soccer,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles