27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Waziri Maliasili ateta na Maafisa uhifadhi

Na Happiness Shayo, WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amekutana na askari wa uhifadhi nchini na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Taifa.

Ameyasema hayo leo katika kikao chake na Askari Uhifadhialipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba Kijereshi lililoko Wilayani Busega, mkoani Simiyu.

“Niwaombe tufanye kazi kwa uadilifu, uwajibikaji na utii katika kulinda rasilimali za Taifa,” amesema Masanja.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja  (katikati) akizungumza na Maafisa na Askari Uhifadhi alipotembelea Hifadhi ya Pori la Akiba  Kijereshi lililoko wilayani Busega mkoani Simiyu

Aidha, amekiagiza Kitengo cha Intelijensia kuhakikisha kinasambaratisha mitandao ya ujangili kwa kuzuia mipango yao yote na kutegua mitego ya ujangili ili kuendeleza utalii.

Pia ameitaka Idara ya Utalii wilayani hapo kuweka mipango thabiti ya kukuza na kuendeleza utalii.

Aidha, Masanja amewataka askari hao kushirikiana na wananchi katika kukabiliana na tatizo la tembo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb) akiangalia mandhari ya Pori la Akiba  Kijereshi lililoko Wilayani Busega mkoani Simiyu. Kushoto kwake ni Meneja wa Pori la Akiba  Kijereshi, Lusato Masinde.

“Tuwe karibu na wananchi kwa kuwaelimisha namna ya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu na pia inapobidi tuwapatie vifaa vitakavyowasaidia kufukuza wanyama hao ”amefafanua Masanja.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Maafisa na Askari Uhifadhi kutoka Pori la Akiba  Kijereshi  na Kikosi dhidi ya Ujangili kutoka Bunda na Mkoa wa Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles