24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: Tutatekeleza maazimio ya SADC

Nora Damian Na Andrew Msechu

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema wamejipanga kuhakikisha maazimio ya mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanatekelezwa ili kutomwangusha Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kufungwa kwa mkutano huo, Bashe alisema mkakati wa viwanda wa SADC utafanikiwa kutokana na kuwapo uwekezaji katika sekta ya kilimo.

Alisema wamechukua hatua mbalimbali kama kupitia upya sera ya kilimo, kumwondolea vikwazo mkulima na kupunguza gharama za uzalishaji ili waweze kutumia fursa zilizopo katika soko la SADC.

“Rais Magufuli ametoa mwongozo wa namna gani SADC itafanya kazi kwa mwaka huu mmoja, jumuiya hii ina idadi ya watu zaidi ya milioni 300, hii ni fursa kwa wakulima kwani kuna uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula.

“Naziomba sekta binafsi zichangamkie fursa hii kwa sababu Serikali haina mashamba, wanaolima ni wananchi mmoja mmoja, kama wizara tumeanza mchakato wa kupitia upya sera ya kilimo iendane na mahitaji ya kisasa.

“Tunaangalia maeneo ambayo mwanzo yalikuwa hayatiliwi mkazo, tumekuwa na lugha za kusema kilimo ni cha kujikimu, kimegawanyika maeneo makubwa zaidi ya matatu, kuna maeneo ya mbogamboga na mazao ya matunda, tunayatengenezea utaratibu ambao utashirikisha sekta binafsi kwa kiasi kikubwa,” alisema Bashe.

Alisema mpango wa kumwondolea mkulima vikwazo, unalenga kumruhusu kuuza mazao yake pale ambapo kuna soko na wanapitia mfumo wa ushirika ili kuwainua wakulima wadogo wadogo.

 “Watu wa sekta binafsi njooni wizarani na pale ambapo tunadhani kuna mkwamo wa kiutaratibu tunapitia upya sera na sheria zote zinazosimamia bodi za mazao ili kuifanya sekta ya kilimo iwe rafiki,” alisema.

Alisema pia wameandaa kongamano kubwa la wazalishaji wa mazao ya chakula litakalofanyika Agosti 29 – 30 la namna ya kuendeleza sekta ya kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles