23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe amaliza urasimu kuiuzia Kenya tani milioni moja za mahindi

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameanza kazi rasmi kwa kufumua urasimu wa biashara ya nafaka kati ya Tanzania na Kenya, huku akiagiza makubaliano ya nchi hiyo jirani kuuziwa tani milioni moja za mahindi na unga yasainiwe kabla ya wiki ijayo kwisha.

Bashe alitoa maagizo hayo katika kikao na Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo wa nchi ili kuwezesha Tanzania kuiuzia nchi hiyo mazao ya chakula, hususan mahindi.

Aliagiza kuchukuliwa hatua za kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha usafirishaji mazao kwenda nchini humo ikiwamo kufanyika utaratibu utakaomwezesha mfanyabiashara atakayenunua mahindi kutoka katika vituo vitakavyotengwa kupewa taarifa itakayomwezesha kuyasafirisha moja kwa moja bila kulazimika kukaguliwa tena njiani.

“Kama kutakuwa na ‘seal’ ambayo tutaiwekeza kwenye stoo zetu ili njiani asichanganye mazao yetu na mazao ‘sub standard’ ifanyike kule kule, kwa hiyo mtu aliyeko ‘border’ ajue kabisa mahindi haya yanatoka Sumbawanga yanaenda Nairobi, gari iliyopakia ni ‘plate’ namba kadhaa, kwenye gunia kumefungwa ‘seal’ yenye ‘serial’ namba hizi,” alisema Bashe.

Alisema kwa sasa kumekuwa na usumbufu mwingi kwa wafanyabiashara wanaosafirisha mahindi kwenda Kenya ambao wamekuwa wakilazimika kukaguliwa mara kwa mara huku wengine wakikwama mpakani kwa muda mrefu.

Kutokana na hali hiyo, aliagiza wiki ijayo kifanyike kikao kitakachoshirikisha Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), PHS, Idara ya Usalama wa Chakula, Wakala wa Hifadhi za Chakula (NFRA) na Baraza la Nafaka Afrika Mashariki ili wafanyabiashara wa Tanzania waweze kuweka taarifa zao kurahisisha upatikanaji wa mikataba badala ya mtu kusafirisha mzigo bila kuwa na mkataba kule anakokwenda na kuondoa usumbufu.

Bashe alisema nchi hizo mbili zimekubaliana kuuziana mahindi ambapo Kenya imesema uhitaji wake ni tani milioni moja kwa kipindi cha mwaka mmoja, kiasi ambacho Bodi ya Mazao Mchanganyiko imethibitisha kwamba inao uwezo wa kuhudumia.

Alisema wamekubaliana katika kila kituo cha mauzo ni lazima mamlaka kama vile TBS, Atomic na PHS wawepo ili mfanyabiashara anapotoka pale kwenye kituo na mzigo wake, anaondoka moja kwa moja bila kulazimika kusimama sehemu yoyote kukaguliwa.

Pia alisema hategemei Mkurugenzi wa Bodi ya Mazao Mchanganyo naye ‘ata-behave’ kama lile Shirika la Taifa la Usagishaji na alimtaka kuhakikisha kama wafanyabiashara kutoka Kenya watatuma barua pepe azijibu haraka hata kama ni usiku.

“Balozi wa Kenya atachukua mawasiliano, atakuwa anawasiliana na wewe kama mfanyabiashara yeyote anakuwa anahitaji kufanya biashara na sisi,” alisema Bashe.

 “Jambo jingine ambalo tumekubaliana hapa, ni kwamba watu wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko kwa kuwa wao wanazalisha dona, mambo makubwa mawili, timu inayokuja itupe mahitaji ya dona kiasi gani itahitaji ili ‘traders’ (wafanyabiashara) waje wanunue ‘all ready value added product’ (bidhaa ambazo tayari zimeongezwa thamani).

“Watatumia ‘facility’ (miundombinu) za Bodi ya Mazao Mchanganyiko kwa ajili ya ‘processing’, kusafisha na ‘packing’ (kufungasha) kwa sababu tunataka bidhaa ikitoka Tanzania isiwe tu kwenye magunia ya kawaida, ‘iki-cross border’ (ikivuka mpaka) iwe ‘branded as a Tanzanian product’ (inajionesha kuwa ni bidhaa ya kitanzania).

“Ndiyo maana tunawataka watu wa Kenya Bureau of Standard (Shirika la Viwango Kenya) waje na watu wa TBS wakae pamoja ili tukubaliane ‘framework’ ya ‘quality controls’ (viwango vya ubora). ‘Ku-harmonize’ (kurahisisha) haya mambo tuondoe hiyo vikwazo vilivyopo.

“Katikati ‘price’ (bei) tumeshawapa, hatuitangazi kwa sababu inaweza ikaleta migogoro sokoni, wakulima wakiisikia na wenyewe wanapanda itakuwa balaa. ‘Tumesha-mention price’ (tumeshataja bei) ya unga, ya mahindi,” alisema Bashe.

Pia aliitaka Idara ya Masoko ya Wizara ya Kilimo kushiriki kikao na kuhakikisha inaorodhesha kampuni zote zinazozalisha unga hapa nchini ili ziweze kusajiliwa ili wakifikia viwango waweze kuuza moja kwa moja nchini humo.

“Siyo kwa kuwatoza hela, jamani mtu wa wizara anayehusika siyo sasa hivi nasema, tuanze ‘ku-introduce fee’ (kuanzisha tozo). Kwa sababu wapo Watanzania wanazalisha sembe hapa wanahitaji kuuza sembe yao Kenya. Kwa hiyo ni vizuri watu wetu wa wizara ‘tu-facilitate’ hiyo.

 “Wewe NFRA hizo kilo milioni mbili zilizopo ‘immediately you can tell your people’ (muda mfupi kuanzia sasa unaweza kuwaambia watu wako) kwa ajili ya kuchukua katika ‘point’ ya Makambako na Songea tuanze kuuza hizo,” alisema Bashe.

Pia aliagiza kusainiwa kwa mkataba wa kuuziana kiasi hicho cha mahindi cha tani milioni mbili kwa mwaka mmoja na pande zote, NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko wahakikishe wanashirikiana kupatikana kiasi hicho.

“Lakini hata ‘traders’ wa kitanzania ambao wanataka kuuza wawe ‘facilitated’ (wawezeshwe) waweze kwenda kuuza moja kwa moja Kenya,” alisema.

Aliitaka NFRA na taasisi nyingine za Serikali kuanza kufikiri kibiashara kwa jinsi gani ya kutengeneza faida ili ifike mahali waache kuitegemea Hazina kuwapa fedha kwa ajili ya akiba kwa sababu wanazalisha faida yao wenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles