24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe agawa trekta 400, pikipiki 1,000 na baiskeri 2,500 kwa wakulima

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakulima wa zao la Pamba nchini wanatarajia kunufaika na zana za kilimo kufuatia ugawaji wa trekta 400, pikipiki 1,000 na baiskeli 2,500, boza 58 kwa ajili ya viuatilifu vya dawa na mbolea hai lita 3,000.

Zana hizo zimekabidhiwa na Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo kufuatia ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora tarehe 11 Septemba 2024.

“Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inalenga kuendelea kuwekeza kwa wakulima ili wazalishe mazao kwa tija. Na tutaendelea na mpango wa kuchimba mabwawa ili waanze pia kuvuna maji ya mvua na kuwa na Kilimo cha umwagiliaji,” amesema Waziri Bashe.

Ameongeza kuwa ni vyema wakulima hao kutumia ipasavyo fursa na nyenzo hizo za kilimo na kupuuza baadhi ya wanasiasa.

“Serikali hii haiwezi kutoa dawa feki, mbegu feki na wanunuzi feki kwa wakulima. Siasa zinaleta uchochezi kwa wakulima zinaharibu maisha ya watu na hilo sitoruhusu huo mchezo kwenye Sekta ninayosimamia,” amesema Waziri Bashe.

Amefafanua zaidi kuwa “hatuwezi kuwa na Taifa linatukana watu, linatukana Serikali tunakaa kimya. Watu walikuwa na mateso walikopwa, pamba zilidoda. Miaka miwili tumetoa ruzuku ya mbolea bure na tutaendelea kufanya hivyo na tutaendelea kununua mazao.” Pia ameeleza nia ya wizara kuweka kituo cha ununuzi wa nafaka Wilayani Igunga.

Aidha, Mhe. Waziri Bashe ametumia fursa hiyo kueleza mipango ya Serikali ya kujenga mabwawa na miundombinu ya umwagiliaji ya kutosha Igunga kwa kuwa kitakwimu ni ya kwanza au ya pili, hivyo ni lazima kuwa na uzalishaji wa uhakika kwa kilimo cha umwagiliaji cha Pamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles