23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Basata yamsajili bure msanii aliyetembea kwa miguu

basata eNA MWANDISHI WETU

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limempongeza na kumpa usajili wa bure msanii, Joseph Stanford, aliyetembea kwa miguu umbali wa zaidi ya kilomita 1,200 kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Stanford alitembea kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kwa lengo la kupongeza utendaji na uundaji wa Idara ya Sanaa iliyo chini ya Wizara ya Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Rais Magufuli.

Kutokana na kujitoa huko kwa nchi, Basata imemsajili bure msanii huyo ili atambuliwe rasmi katika tasnia ya sanaa na baadaye kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za sekta hiyo.

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema Stanford ameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yake kwani haikuwa kazi rahisi kutembea umbali mrefu usiku na mchana hadi kufika na kumpongeza Rais Magufuli.

“Sisi kama Baraza tunafarijika sana, tunafurahi kuona wasanii na vijana kwa ujumla mnakuwa wazalendo na kufurahishwa na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano. Tunafurahi zaidi unapopeleka ujumbe wa wasanii kwamba wamefurahia kuundwa kwa idara ya sanaa,” alisema.

Naye Stanford alifurahishwa na mapokezi ya Basata lakini alisisitiza kwamba ndoto yake ni kumfikishia salamu za pongezi Rais Magufuli huku akiamini kwamba atapata mafanikio kupitia kazi za sanaa.

Msanii Stanford anatokea eneo la Mabatini jijini Mwanza na ametembea kwa siku 25 kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam na ametumia kiasi cha shilingi 45,000 pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles