30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu azivalia njuga tiketi za elektroniki

waziri majaliwaNA NYEMO MALECELA, DAR ES SALAAM

MATUMIZI ya tiketi za kawaida kwenye viwanja vya soka nchini yanatarajiwa kufika mwisho mara baada ya mchezo wa Simba na Yanga utakaochezwa keshokutwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kumuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kuhakikisha tiketi za kielektroniki zinatumika kwenye mechi zote za soka zitakazochezwa kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo ili kupunguza ubadhirifu wa mapato ya milangoni ambao umekuwa ukijitokeza kila kukicha kutokana na matumizi ya tiketi za kawaida kutoa mianya ya fedha hizo kutumika vibaya.

“Tuna wataalamu wa kutosha hivyo zoezi la kutumia tiketi za elektroniki linatakiwa kuanza mara moja na ikiwezekana zoezi la mashabiki kununua tiketi kupitia simu zao liwe linaanza wiki moja kabla ya mechi,” alisema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amelishangaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka kumrudisha kocha wa zamani wa Taifa Stars, Kim Poulsen kuwa kocha wa timu ya Taifa za vijana.

Majaliwa alihoji kwanini TFF inataka kumrudisha Poulsen wakati awali ilimfukuza wakati akiinoa Taifa Stars, huku akiuliza ni vigezo gani wanatumia kumuona sasa anafaa kufundisha timu ya taifa za vijana.

“Kama mnamrudisha (TFF) inabidi TAFCA (Chama cha Makocha Tanzania) ipitie upya mkataba wake ili kujiridhisha kama ana vigezo vya kuifundisha timu hiyo ya vijana,” alisema Waziri Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles