28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Jux: Nilianza kuwa staa kabla ya Vanessa

Jux-n-vee-1NA JOHANES RESPICHIUS

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Musa ‘Jux’, amesema alianza kupata umaarufu kabla ya mpenzi wake, Vanessa Mdee, hivyo si sahihi kudai kwamba anatembelea nyota ya mrembo huyo kwenye sanaa ya muziki.

Akizungumza na MTANZANIA, Jux alisema kama alikuwa anataka kufahamika kupitia Vanessa wangeshafanya wimbo wa kushirikiana kwa kuwa ni wapenzi kwa sasa.

“Nilianza kufanya muziki na kupata umaarufu kabla ya Vannesa, hivyo mimi nilianza kuwa staa kabla yake ila yeye anaonekana staa kwa kuwa anajituma zaidi ya wasichana wengine na pia anafanya muziki mzuri kuliko wasichana wengine na nafasi yake ya ushindani na wasanii wenzake ni ndogo hivyo yeye anaonekana zaidi kuliko wengine, uhusiano wetu usitumiwe kupotosha hilo na ndiyo maana kwenye maonyesho au mahojiano ni vigumu kutuona pamoja,” alisema Jux.

Jux aliongeza kuwa anavutiwa na Vanessa kwa sababu anajituma na anampa changamoto ya kutafuta mafanikio kila siku ndiyo maana Vanessa ni mwanamke bora kwake.

“Mimi napenda changamoto kwa kuwa napenda kuwa tajiri ndiyo maana najiwekeza sana katika biashara mbalimbali ili nitimize ndoto zangu na suala la mtoto bado miaka minne hivi,” anaeleza Jux mwenye miaka 26.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles