22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Barcelona watwaa Kombe la Dunia Japan

BarcelonaYOKOHAMA, JAPAN

KLABU ya Barcelona imeibuka mabingwa katika michuano ya klabu ya dunia iliyokuwa ikiendelea nchini Japan baada ya kuifunga River Plate ya Argentina mabao 3-0, kwenye Uwanja wa Nissan Stadium.

Katika mchezo huo, mshambuliaji hatari wa Barcelona, Luis Suarez, alikuwa mwiba kwa mabeki wa River Plate, ambapo alipachika mabao mawili huku Lionel Messi akiwa wa kwanza kupachika bao.

Hata hivyo, katika mchezo wa nusu fainali, Suarez alionesha umahiri wake kwa kupachika mabao matatu peke yake dhidi ya Guangzhou Evergrande, huku washambuliaji wenzake, Messi na Neymar wakiwa nje majeruhi.

Barcelona imekuwa klabu ya kwanza duniani kuchukua taji hilo mara tatu.

Kwa matokeo hayo, Barcelona wanazidi kujikusanyia mataji mwaka huu huku likiwa la tano, wakati mataji mengine ni pamoja na Ligi Kuu Hispania, Copa del Rey, Ligi ya Mabingwa na Uefa Super Cup.

Katika michuano hiyo mabingwa kutoka barani Afrika, TP Mazembe kutoka nchini Congo (DRC), walitolewa mapema dhidi ya Club America ambapo Mazembe walipokea kichapo cha mabao 2-1 na kuzizima ndoto za Watanzania wanaokipiga katika klabu hiyo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ya kufika fainali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles