24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Balotelli aibakisha Nice kileleni

mario-balotelliNICE, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Nice, Mario Balotelli, anazidi kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu nchini Ufaransa, baada ya juzi kufunga bao lake la sita katika michezo mitano aliyoicheza.

Klabu hiyo ya Nice kwa sasa inashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi, ikiwa na alama 29 baada ya kucheza michezo 11, ikiwa mbele kwa alama sita dhidi ya wapinzani wake Monaco ambao wana alama 23.

Katika mchezo wa juzi, Nice iliisambaratisha Nantes kwa mabao 4-1, huku Balotelli akifunga bao moja na kuonesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo.

Balotelli alionekana hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Liverpool, hivyo kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp, alimwambia kwamba atafute timu kwa kuwa katika kikosi chake hana nafasi.

Mchezaji huyo alikuwa katika klabu ya AC Milan kwa mkopo akitokea Liverpool, hivyo mara baada ya kumalizika mkataba wake kwa mkopo, alirudi Liverpool lakini alikosa nafasi kabla ya Nice kuamini kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho.

Uongozi wa klabu ya Nice unaamini kuwa Balotelli anaweza kufanya makubwa zaidi ndani ya klabu hiyo tofauti na yale ambayo aliyafanya misimu iliopita akiwa nchini England.

Monaco wanashika nafasi hiyo ya pili baada ya kutoka sare ya bao1-1 dhidi ya St Etienne, wakati huo mabingwa watetezi wa Ligi hiyo PSG, wao wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 23 tofauti na mabao ya Monaco.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles