31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Conte awataka Chelsea wasiangalie msimamo wa Ligi

antonio-conteLONDOND, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte, amewataka wachezaji wake wasiangalie msimamo wa Ligi kwa sasa hadi baada ya siku kuu ya Krismasi.

Timu hiyo juzi ilishuka dimbani na kufanikiwa kushinda mabao 2-0 dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa St. Mary.

Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea ni klabu pekee ambayo imeshinda katika Uwanja wa St. Mary dhidi ya Southampton.

Hata hivyo, katika mchezo wa juzi Chelsea imefanikiwa kushinda mara nne mfululizo, hivyo Conte anaamini kuwa hiyo ni dalili nzuri kwa klabu hiyo kuendelea kufanya vizuri kwa michezo ijayo.

Kocha huyo ameimwagia sifa safu ya ulinzi ya klabu hiyo kwa michezo minne iliyopita pamoja na safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Diego Costa na Eden Hazard.

Kocha huyo amewataka wachezaji kwa kushirikiana na wachezaji wengine kuendelea na kazi wanazozifanya bila ya kuangalia nafasi waliopo kwa sasa.

“Kwa sasa hakuna umuhimu wowote wa kuangalia nafasi tuliopo katika msimamo wa Ligi, kila mmoja anajua kwamba tupo sehemu mzuri lakini haina umuhimu kwa sasa, kikubwa ni kuendelea kujituma kwa hali na mali kwa ajili ya kuzidi kupiga hatua.

“Kwa sasa ninaangalia kila mchezo uliopo mbele yetu na ninaamini tupo katika mazingira mazuri na kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kusonga mbele.

“Kitu ambacho nitaendelea kuwasisitizia wachezaji wangu ni kujituma zaidi kwa ajili ya kutimiza malengo yetu kwa kuwa safari bado ni ndefu.

“Ili tuwe na uhakika wa kuchukua ubingwa ni lazima tukashinda michezo mingi, lakini kwa sasa siwezi kusema kama tunaweza kuchukua ubingwa kwa kuwa bado ushindani ni mkubwa sana,” alisema Conte.

Kwa sasa Chelsea inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi huku ikiwa na alama 22, baada ya kucheza michezo 10, wakati Man City ikishika nafasi ya kwanza ikiwa na alama 23.

Conte amedai kuwa baada ya siku kuu ya Krismasi wachezaji wanaweza kuangalia wapi walipo lakini wanaweza kuwa na furaha kama wataweza kujituma kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles